KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, July 9, 2014

Klose ndiye mfungaji mabao mengi zaidi ya kombe la dunia 16.

Klose ndiye mfungaji mabao mengi zaidi ya kombe la dunia 16.
Mshambulizi wa Ujerumani Miroslav Klose ameweka rekodi ya kuwa mfungaji mabao mengi zadi katika historia ya kombe la dunia.
HILI NDILO BAO LA KLOSE LA KIHISTORIA LILILOVUNJA REKODI YA RONALDO DE LIMA LIMA
Klose alifunga bao la pili Ujerumani ilipoiangamiza Brazil mabao 7-1 katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la dunia huko BELO HORIZONTE, Brazil.
Klose mwenye umri wa miaka 36 amefunga sasa jumla ya mabao 16 baada ya kushiriki michuano minne ya kombe la dunia.
Klose amefunga mabao 16
Pole: Miroslav Klose aliyefunga goli la pili la Ujerumani akimfariji Luis Gustavo baada ya kumalizika kwa mchezo
 Mshambulizi huyo alikuwa ametoshana na mshambuliaji wa zamani wa rekodi hiyo mbrazil Ronaldo de Lima alipoifungia Ujerumani bao la pili la kusawazishia dhidi ya Ghana katika mechi za mchujo awali katika fainali hizi.
Klose amefunga mabao 16.
Wakati huohuo mshambulizi huyo amevunjilia mbali rekodi ya mfungaji mabao mengi zaidi ya kimataifa kwa mjerumani alipoifungia timu yake bao la 68 Ujerumani ilipokuwa ikishiriki mechi ya kirafiki dhidi ya Armenia.
Rekodi ya awali ya Ujerumani ilikuwa inashikiliwa na Gerd Mueller
Kufuatia Ushindi huo Ujerumani imefuzu kwa fainali yake ya kwanza katika kipindi cha miaka kumi na miwili iliyopita.