KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, July 9, 2014

Ukiona mtu mzima analia ujue kuna jambo, Luiz machozi chapachapa baada ya kichapo cha karne na wamewakubali mziki wa Wajerumani ulikuwa si wa kitoto.

Kilio cha mtu mzima: Liuz akibubujikwa na machozi baada ya kichapo cha maangamizi kutoka kwa Ujerumani
 Nahodha wa muda wa Brazil David Luiz amewataka mashabiki wa tim,u hiyo kote duniani kuwasamehe wachezaji waliokuwa uwanjani Selecao ilipoadhibiwa kichapo cha mabao 7-1 na Ujerumani katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la dunia huko Brazil.
Amini Usiamini Ujerumani ilikuwa inaongoza mabao 5-0 kufikia dakika 29 ya kipindi cha kwanza .
"Wajerumani walikuwa timu bora zaidi yetu''
Luiz,ambaye alitajwa kama nahodha wa muda baada ya marufuku ya Nahodha Thiago Silva kumlazimu kutizama tu mechi hiyo alisema hawjui kilichotendeka lakini ni wakati wao kujifunza kutokana na aibu hiyo ya kusakamwa 7-1. "Ni siku ya majonzi tele kwa wabrazil''.
Luiz akilia baada ya kushindwa na Ujerumani

"Mtuwieni radhi sijui tutafanya nini ilituwaone tena wabrazil wakitabasamu,?
Kilio kimezidi kote nchini humo haswa baada ya nyota wa Brazil Neymar kujeruhiwa uti wa mgongo Ijumaa iliyopita katika mechi ya kufuzu kwa nusu fainali dhidi ya Colombia.
Kwa Upande wake Kipa wa Brazil Julio Cesar alitaja dakika hizo kumi timu hiyo ilipofungwa mabao manne kuwa sawa na kuzimia.
''Sio jambo unaloweza kujieleza.
Julio Ceasar; Ujerumani ilikuwa timu bora

Kombe hili la dunia limekuwa lenye ufanisi hadi leo.
Hata hivyo tunawashukuru Wabrazil kwa kutuunga mkono katika kipindi hichi chote .
Hata wachezaji wakiomba msamaha kwa kichapo hichi cha leo ,ni wazi kuwa mjerumani alituzidi maarifa .
Lazima tukali hilo walikuwa bora kutuliko leo.'''