KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, July 8, 2014

Afisa wa Match Hospitality akamatwa

Afisa wa Match Hospitality akamatwa Brazil
Maafisa wa polisi nchini Brazil wamemkamata afisa mkuu mtendaji wa kampuni mshirika wa FIFA kwa tuhuma za uuzaji tiketi za kombe la dunia kinyume na kanuni.
Ray Whelan ambaye ni meneja mkuu mtendaji wa kampuni mshirika wa FIFA Match Hospitality alikamatwa katika hoteli moja huko Rio de Janeiro , inayotumika pia na maafisa wa shirikisho la FIFA.
Juma lililopita watu wengine 11 walikamatwa kwa kuuza tiketi za kombe la dunia kinyume na kanuni za FIFA .
Polisi walisema kuwa kikundi hicho kilikuwa sehemu ya genge kubwa la kimataifa ambalo lilikuwa likiuza tiketi ambazo zilikuwa zimetengewa makundi maaluma ikiwemo tiketi zilizokuwa zimetengewa wachezaji .
Afisa wa Match Hospitality akamatwa Brazil

Polisi nchini Brazil walisema kuwa tayari genge hilo lilikuwa limetia kibindoni takriban dola milioni 90 katika mauzo hayo ambayo yamekuwa yakiendelea katika mashindano manne ya kombe la dunia .
Kufuatia kashfa hiyo uchunguzi unaendelea kubaini iwapo baadhi ya tiketi hizo zimeuziwa watalii ambao hawakujua walikuwa wanakiuka sheria za shirikisho la soka duniani FIFA.
Kompyuta na vifaa vyengine vya kielektroniki vilikamatwa na polisi kwa uchunguzi zaidi kutopka kwa mkahawa huo wa kifahari ulioko Copa Cabana Palace Hotel
Kampuni hiyo ya Match Hospitality yenye makao yake huko Switzerland hadi sasa haijatoa taarifa zozote kufuatia ugunduzi huo.
Afisa anayeongoza uchunguzi huo Fabio Barucke, amesema kuwa afisa huyo alikuwa na hati zinazomruhusu kuingia katika afisi zote za fifa kwa hivyo alikuwa na uwezo wa kuzipata tiketi hizo.
Uchunguzi unaendelea.

No comments:

Post a Comment