KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, July 8, 2014

Samuel Eto’o bado anaranda Ulaya kurejea tena nchini Italia mara hii ni AS Roma endapo mambo yatakwenda poa

Samuel Eto’o kuelekea Italia
KLABU ya AS Roma ya Italia imeanza mazungumzo na wawakilishi wa Samuel Eto’o jana ikiwa ni baada ya kukamilisha usajili wa mchezaji mwenzake wa zamani wa Chelsea Ashley Cole.
 Eto’o mwenye umri wa miaka 33 ni mchezaji huru toka aondoke Stamford Bridge na tayari amepata ofa kutoka China na Uturuki lakini mwenyewe anataka kurejea nchini Italia. 
Katika mazungumzo hayo nyota huyo anatarajiwa kupunguziwa mshahara wake kwa kiasi cha paundi milioni tatu ikiwemo na posho.
 Kama akifanikiwa kutua Roma atakuwa amejiunga na mchezaji mwenzake kutoka Chelsea, Cole aliyesaini mkataba wa miaka miwili na timu hiyo huku ikiwa ni mara ya pili kwa nyota huyo kurejea nchini Italia baada ya kuitumikia Inter Milan kati mwaka 2009 na 2011.