KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, July 15, 2014

Liverpool na Lazar Markovic kufunga ndoa leo ambapo Brendan Rogers atakuwa akiandikisha usajili wa nne kiangazi hii

Markovic akiwa na jezi ya Liverpool
Lazar Markovic hii leo atakuwa akifanyiwa vipimo vya afya kabla ya kuanguka saini ya kumalizia uhamisho wake wa kujiunga na Liverpool wenye thamani ya pauni milioni £60 ambapo anatarajiwa kuthibitishwa na meneja wa klabu hiyo Brendan Rodgers kuwa usajili wake mkubwa wa majira haya ya kiangazi.
Nyota huyu wa kimataifa wa Serbia aliwasili Merseyside Jumapili usiku kabla ya kumalizia vipimo vya afya kwenye zahanati ya Spire na eneo la kufanyia mazoezi la klabu hiyo Melwood baada ya Liverpool kukatisha mkataba wake na Benfica wakitumia pauni milioni £20.
Markovic aliwasili  Anfield na baadaye akionekana kupiga picha akiwa na jezi ya Liverpool.

Liverpool ilikuwa ikimfukuzia Markovic kiangazi yote hii na alikuwa katika mipango yao kwa muda mrefu kabla hata ya taarifa kuwa mshambuliaji wao Luis anataka kujiunga na Barcelona na baada ya taarifa hizo ndipo wakachangamka kumnasa nyota huyo kijana ambaye anadhaniwa kuwa mchezaji kijana mwenye thamani kubwa barani Ulaya.

Markovic, ambaye alifanya kazi kubwa kuisadia Benfica kushinda taji la ligi ya Ureno msimu uliopita amekubali kimsingi mkataba wa muda mrefu ndani ya viunga vya Anfield na kuungana na Rickie Lambert, Adam Lallana na Emre Can kama wachezaji wapya ndani ya Anfield ambao walimaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Manchester City katika ligi ya England mwezi May mwaka huu.
Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers amekuwa yuko bize sana kiangazi hii kusaka wachezaji wapya.