KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, July 15, 2014

Baada ya fainali ya kombe la dunia: Blatter na Maradona wamkataa Lionel Messi

Akikabidhiwa: Rais wa FIFA Sepp Blatter wakati akikabidhia tuzo ya Golden Ball kwa Messi lakini baadaye akaonekana kushangazwa na tuzo.
Hakustahili! Diego Maradona amesema tuzo ya Messi ilikuwa ni mipango ya kibiashara

Lionel Messi amejikuta katika wakati mwingine mgumu baada ya kumalizika kwa fainali za kombe la dunia hususani hapo jana kufuatia nguli mwingine wa sona duniania mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina Diego Maradona na Bosi mkubwa kabisa wa soka duniani Sepp Blatter kushangazwa na tuzo na tuzo yake ya mchezaji aliyevutia kwenye kombe la dunia.
Messi alionekana hakuwa na lolote alilolifanya kulinganisha na wachezaji wengine baada ya Argentina kufungwa na Ujerumani bao 1-0 katika dakika za nyongeza uwanja wa Maracana, na kisha kuzawadiwa tuzo ya Golden Ball.

Mshituko umekuja huku ikidhaniwa pengine walikuwepo wengi waliong'ara zaidi nyuma yake akiwemo winga wa Uholanzi Arjen Robben au mfungaji wa michuano hiyo kutoka Colombia James Rodriguez aliyefunga magoli sita ambaye licha ya kushinda tuzo ya Golden Boot pengine angestahili pia Golden Ball ambaye kimsingi Maradona ameonekana kumkubali sana.

 Ilikuwa ni timu ya watu wa kiufundi ya FIFA ambayo ilimchagua Messi ambapo baadaye ikaonekana pengine msuli wa kiushindani wa kibiashara ulitumika kwa watengenezajiwa wa vifaa vya michezo vya Adidas ambao walidhamini tuzo ya mshindi wa Golden Ball ambapo waliamtaka Messi kwa kuwa ni sura ya dunia katika kuitambulisha bidhaa yao.

No comments:

Post a Comment