KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, July 15, 2014

Kamati ya usajili Simba: Tunamtafutia Kocha Logarusic washambuliaji wawili na kiungo mchezeshaji kutoka Nigeria, Afrika kusini na Rwanda.

Makamu mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu ya Simba Kassim Mohamed Dewji
Kamati ya usajili ya klabu ya Simba imesema bado inaendelea na mchakato wa usajili wa klabu hiyo na kwamba mchakato unaendelea kwa kusaka wachezaji watatu wa kigeni muhimu yakiwa ni maelekezo ya kocha mkuu wa klabu hiyo Mcroatia Zdravko Logarusic.

Akiongea na Rockersports katika mahojiano maalumu makamu mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo Kassim Mohamed Dewji amesema kocha mkuu wa klabu yao ameiagiza kamati yake imtafutie wachezaji wanne muhimu na atumie kipindi hiki cha maandalizi ya kuanza kwa msimu kuwajaribu kabla ya kuamua ni yupi anafaa kuisaidia Simba.

Dewji ambaye ni katibu wa zamani wa klabu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi amesema kocha Logarusic anatafuta wachezaji wawili washambuliaji wa kigeni ambao wana uwezo tofauti ukilinganisha na washambuliaji wa Tanzania, mlinzi wa kushoto na kiungo mchezeshaji mwenye nguvu na uwezo wa kumiliki vizuri mpira. 

Amesema tayari ombi la kocha Loga la golikipa limesha fanikiwa kwa kumsajili Husein Sharif 'Casillas' kutoka Mtibwa ambaye amekuwa akivutiwa naye na sasa ametua Msimbazi, na sasa kifuatacho wao kama kamati ikiongozwa na mwenyekiti Hans Poppe wanaendelea na zoezi hilo

Amesema tayari kamati yake imeshapokea maombi kutoka kwa mawakala wa nchini tofauti tofauti wa ndani na nje ya nchi zikiwemo nchi za Nigeria, Afrika Kusini na Rwanda ambapo kamati imewaagiza mawakala wa wachezaji hao kuwaleta nchini wachezaji wao wafanye majaribio ndani ya kipindi hiki kilicho salia ambapo kocha Loga ataamua yupi atamfaa kikosini msimu ujao wa 2014/15.

Tayari mchezaji  Dani Van Wyk kutoka Afrika kusini ameshawasili kwa majaribio huku wachezaji wengine wakitarajiwa kuwasili wakati wowote kuanzia sasa.

Dewji amesema kamati ya usajili inafanya kazi yake kwa umakini mkubwa sana na kwamba wanatarajia kufanya usajili mzuri na wenye matokeo mazuri kwa wana Simba.

Kuhusu usajili wa wachezaji Vijana, Dewji amesema usajili wanao ufanya ni kwa mahitaji ya sasa na ya baadaye ambapo bila shaka watahitaji damu changa leo ili kesho wawe wazoefu na kwamba wana Simba watambue kuwa usajili unaofanywa na kamati yake ni wa kisayansi zaidi na wala si wa kukurupuka.