KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, July 14, 2014

Nadir Haroub Canavaro:Sijakutana bado na kocha Maximo Yanga nina hamu naye sana

 Nahodha na beki wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na Yanga Afrika Nadir Haroub Canavaro amesema ana hamu kubwa ya kukutana na kocha wake mpya katika klabu yake ya Yanga na kwamba anashindwa kujiunga na kikosi cha klabu yake ambacho kipo chini ya kocha Mbazil Marcio Maximo kwa kuwa anajukumu kubwa la kitaifa.

Akiongea na Rockersports moja kwa moja kutoka kambini Tukuyu mkoani Mbeya, Kanavaro ameweka wazi kuwa ana shauku kubwa ya kurejea katika kikosi cha Yanga ambacho mbali ya ujio wa kocha Maximo lakini pia kuna nyongeza ya wachezaji wapya akiwemo Coutinho aliyetokea nchini Brazil.

Canavarro ambae kwa sasa yupo mjini Tukuyu sanjarti ya kikosi cha timu ya Taifa, amesema amekuwa na shauku hiyo kutokana na ujio wa kocha Maximo ambaye amekiri anamuhusudu kutokana na falsafa za ufundishaji wake.

Amesema anampenda sana kocha huyo kutokana na mazuri aliyomuwachia kabla hajaachana na timu ya taifa ya Tanzania mwaka 2010, hivyo mambo yatakuwa mazuri msimu ujao.

Anaamini kikosi cha Yanga kitatisha msimu ujao kwakuwa Maximo ni kocha mzuri.