Stanley Victor "Stan" Collymore, |
Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Stanley Victor
"Stan" Collymore, amepinga hatua ya shirikisho la soka duniani FIFA
ya kumpa tuzo ya mchezaji bora wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2014,
mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Andres Messi.
Messi akiwa na tuzo yake ya mchezaji bora wa mashindano ya kombe la dunia |
Collymore, amesema FIFA wamechemka katika maamuzi ya
kumzawadiwa tuzo hiyo, Lionel Messi kutokana na kiwango duni alichokionyesha
katika mchezo wa hatua ya fainali pamoja na michezo mingine ya michuano ya
mwaka huu.
Amesema wapo wachezaji wengi ambao walionyesha uwezo mkubwa
na ilidhihirika wazi huenda wangepewa tuzo hilo, lakini cha kustaajabisha FIFA
kwa kushirikiana na kamati ya mashindano wamemtangaza Messi, ambaye hakuonekana
kama anaitumikia vyema timu yake ya taifa kama anavyokuwa kwenye klabu yake ya
Barcelona.
"Kiwango chake kilikuwa duni, sijaelewa mpaka sasa kwa
nini amekua Messi isiwe mchezaji mwingine kama James Rodriguez, Alexis Sanchez pamoja
na Manuel Neuer” amesema Collymore.
"Hata ingelikua kuna tuzo ya mchezaji bora wa timu ya
taifa ya Argentina ingelikuwa mimi nisingempa Messi, kutokana na kiwango duni
alichokionyesha” Collymore.
Wengi bado wanaamini kuwa pengine tuzo hiyo ingestahili kuchukuliwa na Toni Kroos, Philipp Lahm na Sami Khedira kutoka katika kikosi cha mabingwa huku akiongezwa Arjen RobbenNeymar na hata mshindi wa tuzo ya ufungaji bora (Golden Boot) James Rodrigues na mlinda mlango Manuel Neuer (the Golden Glove winner), Keylor Navas na Sergio Romero.
Mbali na Lionel Messi kutajwa kama mchezaji bora wa fainali
za kombe la dunia za mwaka 2014, zawadi nyingine kama kipa bora imekwenda kwa
mlinda mlango wa timu ya taifa ya Ujerumani Manuel Neuer, huku kiatu cha
dhahabu kikichukuliwa na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Colombia James
Rodriguez.
Zawadi zilizotolewa kwa wachezaji na timu
Adidas Golden Ball - Mchezaji
bora: Lionel Messi (Argentina)
Adidas Silver Ball - Mchezaji
bora 02: Thomas Muller (Ujerumani)
Adidas Bronze Ball - Mchezaji
bora 03: Arjen Robben (Uholanzi)
Adidas Golden Boot – Mfungaji
Bora: James Rodriguez (Colombia)
Adidas Silver Boot – Mfungaji
Bora 02: Thomas Muller (Ujerumani)
Adidas Bronze Boot – Mafungaji
Bora 03: Neymar (Brazil)
Adidas Golden Glove – Kipa
bora: Manuel Neuer (Ujerumani)
Hyundai Young Player Award – Mchezaji bora mwenye umri mdogo: Paul Pogba (Ufaransa)
FIFA Fair Play Award – Timu
yenye nidhamu: Colombia
No comments:
Post a Comment