KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, July 14, 2014

Rihanna na Kansela Markel wakesha na wachezaji wa Ujerumani kwenye pati ya ushindi wa kombe la dunia

Ujerumani ilimaliza kiu yao ya kusubiri kwa miaka 24 kutwaa kombe la dunia usiku wa Jumapili  ambapo wachezaji walikesha kwa furaha kwa kufikia mafanikio hayo.
Goli pekee la Mario Gotze katika muda wa dakika 30 za nyongeza lilipelekea Ujerumani kushinda taji lake la nne na kwa mara ya kwanza kama taifa moja kufuatia kuwachapa Argentina 1-0 uwanja wa Maracana.
Joachim Low na wachezaji wake walikesha wakisheherekea taji hilo jijini Rio de Janeiro baada ya mchezo ambapo waliungana na familia zao na wapenzi wao.
Katika hali isiyotarajiwa mwanamuziki nguli wa kike wa muziki wa Pop Rihanna aliungana nao ambapo alitumia nafasi hiyo kupiga picha na hata kubusiana na wachezaji wa timu hiyo ya taifa.
Kansela wa UJerumani Angela Markel akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu yake ya Taifa baada ya mchezo.
Rihanna akiwa na Mario Gotdze muuaji wa Argentina kwenye pati
Malkia wa muziki wa Pop Rihanna akipiga picha na mvunja rekodi ya ufungaji kombe la dunia Miroslav Klose
Mtu kati: Rihanna akishikilia kombe la dunia akiwa katikati ya wapenzi wake wa muda nyota wa timu ya taifa ya Ujerumani Podolski na Schweinsteiger ambao wamempa kiss la nguvu mashavu yote.
Muda wa kusheherekea: Schweinsteiger akiwa na jezi iliyosainiwa akiwa pamoja na mpenzi wake Sarah Brandner ndani ya pati
Ni tabasamu mwanzo mwisho: Mkurugenzi wa Daimler Dieter Zetsche, kocha mkuu wa Ujerumani Joachim Low na Rais wa IOC Thomas Bach katika picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment