KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, July 14, 2014

Kuelekea mchezo dhidi ya Msumbiji mataifa ya Afrika, Ulimwengu na Samatta kuwasili Jumatano

Thomas Ulimwengu na Mbwana Ally Samatta kuwasili kwa maandalizi dhidi ya Msumbiji
Washambuliaji Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata wa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wanawasili nchini keshokutwa alfajiri (Julai 16 mwaka huu) kwa ajili ya mechi dhidi ya Msumbiji (Mambas).

Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika (AFCON) kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Mambas itachezwa Jumapili (Julai 20 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 Taarifa iliyotolewa na afisa habari na mawasiliano wa shirikisho la soka nchini Tanzania TFF kwa vyombo vya habari imesema kuwa Ulimwengu na Samata watawasili saa 12 asubuhi kwa ndege ya EgyptAir wakitokea Tunisia ambapo timu yao ya TP Mazembe imepiga kambi kwa ajili ya mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika.
 Taifa Stars imepiga kambi Tukuyu mkoani Mbeya ikijiandaa kwa mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi Mahmoud Ashour kutoka Misri.
Stars ikiwa Tukuyu mkoani Mbeya kwa kambi ya maandalizi
 Stars itarejea jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa (Julai 18 mwaka huu) kwa ajili ya mechi hiyo wakati Mambas nao wanatarajiwa kutua siku hiyo hiyo. Mechi ya marudiano itachezwa kati ya Agosti 1 na 3 mwaka huu nchini Msumbiji.