Ripoti nchini Brazil zinasema kuwa kocha wa timu ya taifa ya Brazil,Luiz Felipe Scolari, ameacha kazi kama meneja wa timu hiyo.
Scolari alilaumiwa pakubwa sana kwa timu ya
Brazil kupata kichapo kibaya ilipocheza na Ujerumani ambao wameibuka
mabingwa wa kombe la dunia mwaka huu.
Kichapo hicho kilikuja wakati wa mechi ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani.
Taarifa rasmi huenda ikatolewa baadaye leo na shirikisho la soka la Brazil.
Hivi karibuni Scolari alikaririwa akisema kuwa ataamua mustakabal wake baada ya kombe la dunia.
Kauli hiyo aliitoa baada ya aibu ya kutandikwa mabao 7-1 na Ujerumani katika mechi ya kwanza ya nusu fainali Jumanne iliyopita.
Vyombo
vya habari vilimuandama mno kwa kichapo hicho huku mwenyewe akiahidi kutoa kauli yake baada ya mechi ya kuamua mshindi wa tatu
dhidi ya Uholanzi siku ya Jumamosi ambapo waliambulia kichapo kingine cha bao 3-0.
Kichapo cha bao 7-1 ndicho kilikuwa kibaya zaidi kuwahi kuipata Selecao tangu mwaka wa 1920 Brazil ilipolimwa 6-0 na Uruguay.
Kocha huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 65 alikuwa ameiongoza Brazil
mwaka wa 2002 lakini akondoka na kurejea mwaka wa 2012 kuiandaa timu
hiyo kwa mashindano haya ya nyumbani.
Brazil walikuwa nyuma mabao 5-0 baada dakika 30 ya kipindi cha kwanza kabla ya kukamilisha mechi hiyo mabao 7-1.
No comments:
Post a Comment