Mjumbe wa kamati ya Ufundi ya shirikisho la soka duniani
kote FIFA Gerard Houlier anatarajiwa kuwasilisha hoja binafsi ya kutaka kanuni
za mabadiliko ya wachezaji za michuano ya shirikisho hilo zibadilishwe kutokana
na tathmini aliyoifanya kwenye fainali za kombe la dunia zinazoendelea nchini
Brazil kwa sasa.
Houlier ambaye anakumbukwa na mashabiki wa soka duniani
kote kufuati mchango wake alioutoa wakati wakiwa meneja wa klabu ya Liverpool
ya nchini Uingereza, anejipanga kuwasilisha hoja hiyo kwenye kamati ya ufundi
kabla ya kufikishwa kwenye mkutano mkuu ujao wa FIFA.
Babu huyo mwenye umri wa miaka 66, ameshawishika kuwasilisha
hoja binafsi kwenye kamati ya ufundi ya FIFA baada ya kubaini ipo haja kwa timu
zinazofika kwenye hatua ya mtoano kupewa ruhusa ya kufanya mabadiliko ya
wachezaji zaidi ya watatu.
Amesema katika fainali za mwaka huu, baadhi ya timu ambazo
ziliingia kwenye hatua ya mtoano zilikabiliwa na mtihani wa kucheza pungufu kwa
dakika kadhaa kutokana na wachezaji kuumia, na wakati mwingine wachezaji
walionekana wakiwa wamechoka, hivyo anahisi ipo haja kwa FIFA kutoa nafasi kwa
makocha kufanya mabadiliko angalau kwa mchezaji mmoja.
Hata hivyo Gerard Houlier amesisitiza hoja yake itahusisha
michezo ambayo itaongezewa dakika 30 endapo mshindi hatopatikana ndani ya dakika
90.
Akitolewa mfano wa mchezo wa Ubelgiji dhidi ya Marekani Houlier
amesema mshindi wa mpambano huo alipatikana baada ya faida ya mchezaji wa akiba
Lomelo Lukaku, aliyeingizwa katika dakika 30 za mwisho ili hali kwa upande wa
Marekani kocha Jürgen Klinsmann alikuwa ameshamaliza idadi ya wachezaji wa
akiba kutokana na baadhi yao kuumia kabla ya kuongezwa kwa dakika 90.
No comments:
Post a Comment