Serengeti kucheza na Polisi na Azam fc Chamazi |
Kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka
17 Serengeti Boys kinaendelea na maandalizi ya kujiwinda na mchezo wa kuwania
kufuzu kucheza fainali za Afrika kwa vijana za mwaka 2015 ambazo zimepangwa
akufanyika nchini Niger.
Kocha mkuu wa kikosi cha Serengeti Boys Ababuu Ally Omari
amesema tayari ameshafanya mchujo kwa baadhi ya wachezaji mbao alianza nao
kambi na sasa kinachoendelea na Program ya kawaida ya mazoezi ya kuhakikisha
wanaikabili vyema timu ya taifa ya Afrika kusini.
Ababuu amesema kikosi chake huenda kikapata mchezo wa
kujipama nguvu mwanzoni mwa juma lijalo na baada ya mchezo huo huenda akafanya
maamuzi mengine ya kuwachuja baadhi ya wachezaji.
Ababuu amesema alianza mazoezi na jumla ya wachezaji 44 ambapo kila siku amekuwa akipunguza wachezaji na sasa amesaliwa na wachezaji 29 ambao kati ya hao magolikipa ni 4.
Aidha amesema anatarajiwa kupata mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya Polisi Moro na Ijumaa watacheza dhidi ya Azam fc uwanja wa Chamazi ukiwa ni ushauri wa mshauri wa Ufundi Stewart Hall.
Kumbuka Serengeti Boys wanajiandaa na mchezo dhidi ya timu ya vijana ya Afrika kusini tarehe 19 ya mwezi huu uwanja wa Azam Complex ukiwa ni mchezo wa mchujo wa fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana kabla ya mchezo wa marudiano ambao utafanyika nchini Afrika Kusini kati Agosti 1-3 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment