Kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kinacho ongoza kwa ubora wa viwango vya FIFA |
Kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kilicho shika nafasi ya pili kwa ubora |
Wenyeji wa fainali za kombe la dunia 2014 Brazil washika nafasi ya saba kwa ubora wa FIFA |
Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania kikishika nafasi ya 106 duniani |
Shirikisho la soka duniani FIFA, hii leo limetangaza orodha
ya viwango vya ubora wa soka, ikiwa ni juma moja baada ya kukamilika kwa
fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 huko nchini Brazil.
Orodha hiyo ambayo hutolewa kila mwezi, imezingatia matokeo
ya michezo ya fainali za kombe la dunia, ambapo mataifa makubwa kama Uingereza yameonekana
kutupwa mbali.
Wenyeji wa fainali za kombe la dunia Brazil nao wameonekana
kuanguka kwa kiasi kikubwa, ili hali waliokuwa mabingwa wa fainali hizo mwaka
2010 Hispania wameporomoka kwa kasi ya ajabu wakitokea nafasi ya kwanza.
Mabingwa wapya wa fainali za kombe la dunia, Ujerumani
wamekalia kiti cha orodha hiyo, baada ya kuonyesha kiwango kikubwa walipokuwa
nchini Brazil, ambapo walicheza michezo saba pasina kufungwa mchezo wowote.
Ifuatayo ni orodha kamili ya viwango vya ubora wa soka
duniani kwa mwezi July mwaka 2014.
1. Ujerumani (+1)
2. Argentina (+3)
3. Uholanzi (+12)
4. Colombia (+4)
5. Ubelgiji (+6)
6. Uruguay (+1)
7. Brazil (-4)
8. Spain (-7)
9. Uswisi (-3)
10. Ufaransa (+7)
11. Ureno (-7)
12. Chile (+2)
13. Ugiriki (+1)
14. Italia (-5)
15. Marekani (-2)
16. Costa Rica (+12)
17. Croatia (+1)
18. Mexico (+2)
19. Bosnia na Herzegovina (+2)
20. Uingereza (-10)
AFRIKA MASHARIKI NA KATI
87. Uganda (-1)
95. Kenya (+13)
96. DRC (-12)
106. Tanzania (+7)
109. Rwanda (+7)
126. Burundi (+2)
No comments:
Post a Comment