KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, July 17, 2014

Ramadhani Chombo Lidondo: Naidai Simba shilingi milioni 10 na mshahara wangu wa miezi mitatu wanilipe

Kiungo wa Simba Ramadhani Chombo Lidondo kuendelea kucheza Simba kunahitaji mazungumzo kwanza nipewe changu na Hans Poppe.

 Kiungo wa Simba Ramadhani Chombo Lidondo anaidai klabu ya Simba zaidi ya shilingi milioni 10 za usajili wake pamoja na mshahara wa miezi mitatu wakati huu ambapo mkataba wake unaelekea kufikia ukingoni.
Akiongea na Rockersports Lidondo amesema deni hilo limekuwa kero kwake kiasi kuona kama uongozi wa klabu yake ya Simba inamchezea mapicha picha ambayo hajui hatma yake itakuwa lini.
Mkataba wa Lidondo na Simba utafikia tamati tarehe 5 mwezi Agosti mwaka huu ambapo kwa mujibu wa maelezo yake amesema mpaka sasa zikiwa zimesalia siku chache kabla ya mkataba huo kumalizika hakuna kiongozi hata mmoja ambaye amekuwa akiwasiliana naye kuzungumzia juu mustakabali wa soka lake ndani ya wekundu hao wa Msimbazi. 
Lidondo ajiunga kwa mara ya pili na Simba akitokea katika klabu ya Azam fc Agosti 2012, usajili ambao ulikumbwa na kadhia za hapa na pale kufuatia klabu ya Azam fc kutaka kumtilia kauzibe kabla ya baadaye timu hizo mbili kufikia muafaka.
Amesema viongozi wa Simba wamekuwa wakimuahidi kila mara kumpatia pesa hizo bila ya kutimiza ahadi yao, huku wakiahidi uongozi mpya utalimaliza suala hilo.
Lidondo amesema mchawi mkubwa wa sakata hili la fedha yake ni mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo Zackaria Hans Poppe ambaye ndiye aliyepeleka hundi ya fedha ya malipo yake ya usajili benki ya CRDB ambapo baadaye aligundua kuwa hundi hiyo imefungwa(closed Cheque) huku akiwa amesha chukua kiasi cha shilingi milioni tano na kusalia milioni tano ambazo benki hiyo kwasasa inamdai yeye Lidondo.
Kuhusu kuendelea kuitumikia klabu ya Simba Lidondo amesema hilo ni suala ambalo linahitaji mazungumzo mengine mapya jambalo amelikatia tamaa kwakuwa klabu hiyo imesha onyesha kudharau huduma yake.
 Sakata la Lidondo linawahusu pia wachezaji kadhaa wa klabu hiyo akiwemo mshambuliaji Betram Mombeki na Haruna Shamte huku pia mlinzi wa zamani wa kushoto wa klabu hiyo Amir Maftaha naye akiidai klabu hiyo kongwe hapa nchini.
Lidondo anaidai Simba shilingi milioni 10 ikiwa ni pamoja na mshahara wake wa miezi mitatu.

No comments:

Post a Comment