Mshambuliaji wa Stars Thomas Ulimwengu |
Washambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana
Samata pamoja na Thomas ulimwengu wamewataka watanzania kuwa kitu kimoja katika
kipindi hiki ambapo timu yao ya taifa 'Taifa Stars' inakabiliwa na mchezo muhimu wa
kuwani kufuzu kucheza fainali za Afrika za mwaka 2015 dhidi ya timu ya taifa
ya Msumbiji.
Washambuliaji hao wawili wamesema hayo mara baada ya
kuwasili jijini Dar es salaam tayari kwa kujiunga na wenzao katika maandalizi
ya mwisho ya kuelekea katika mchezo dhidi ya Msumbiji ambao utachezwa mwishoni
mwa juma hili mwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Theomas Ulimwegu wamesema mchezo huo utakua
mgumu kutokana na kila upande kuhitaji kusonga mbele kwenye hatua ya makundi,
hivyo hakuna njia ya mkato zaidi ya wachezaji kufanya kazi ya ziada ya
kuhakikisha wanashinda mchezo huo.
Kwa upande wa Mbwana Samata amesema maandalizi
waliyoyafanya wakiwa na kikosi cha TP Mazembe kilichoweka kambi nchini Tunisia
kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya klabu bingwa barani Afrika, yanatosha
kwenda sambamba na wachezaji wa Stars ambao kwa kipindi kirefu walikua kambini
chini ya kocha kutoka nchini Uholanzi Mart Nooij.
Samata amesema pamoja na kutabiri mchezo mgumu kati ya Tanzania
dhidi ya Msumbiji bado anaamini viwango vya timu zote mbili vinashabihiana.
Katika hatua nyingine timu ya Taifa ya Msumbiji (Mambas) itawasili
jijini Dar es Salaam kesho tayari kwa mpambano wa mkondo wa kwanza wa kuwania
kufuzu kucheza fainali za Afrika za mwaka 2015 dhidi ya Taifa Stars.
The Mambas watatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere saa 7.30 mchana kwa ndege ya LAM
ikiwa na msafara wa watu 37 ambapo kati ya hao, 25 ni wachezaji.
Wachezaji kwenye msafara huo ni Almiro Lobo, Apson Manjate,
Bone Mario Uaferro, Dario Ivan Khan, Edson Sitoe, Eduardo Jumisse, Gelicio
Aurelio Banze, Helder Pelembe, Josemar Machaisse, Elias Pelembe, Isac Carvalho
na Jeffrey Constatino.
Wengine ni Manuel Fernandes, Manuel Uetimane, Mario
Sinamunda, Momed Hagi, Reginaldo Fait, Reinoldo Mandava, Ricardo Campos, Saddan
Guambe, Simao Mate Junior, Soares Victor Soares, Stelio Ernesto, Vando Justino
na Zainadine Junior.
No comments:
Post a Comment