Wachezaji wa timu ya taifa ya Argentina wamekubaliana
kuchangia kiasi cha dola za kimarekani 135,000 katika hospitali inayotoa tiba
ya magonjwa ya saratani huko mjini Buenos Aires.
Wachezaji wa taifa hilo ambao walicheza hatua ya fainali
kwenye michuano ya kombe la dunia, na kukubali kufungwa bao moja kwa sifuri
dhidi ya Ujerumani wamewasilisha mchango huo kwenye hospitali ya Garrahan
wakiongozwa na nahodha na mshambuliaji wao Lionel Messi.
Hospitali ya tiba za kansa nchini Argentina |
Kwa makusudi ya dhati wachezaji wa Argentina walikubaliana
kwa pamoja kuwasilisha mchango huo ambao unatokana na zawadi ya dola za
kimerakani million 25, ambazo wamekabidhiwa na FIFA baada ya kushika nafasi ya
pili kwenye fainali za kombe la dunia za mwaka huu.
Katika ujumbe wa pamoja na wachezaji hao imeonekana kuguswa
na mahitaji ya hospitali hiyo, ambayo kila leo hutoa huduma kwa wagonjwa wa
saratani, hivyo wanaamini mchango wao utasaidia kukidhi baadhi ya mambo
hospitalini hapo.
No comments:
Post a Comment