KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, July 18, 2014

Serengeti Boys piga hao Amajimboz kwa idadi kubwa ya mabao iwe hazina kabla ya marudiano

Serengeti Boys kuinyoa Amajimbos ya Afrika kusini leo?
Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, Hababuu Ali Omari amesema morali ya wachezaji wake ipo juu kwa ajili ya mchezo dhidi ya Afrika Kusini (Amajimbos) utakaochezwa kesho kwenye uwanja wa Azam Complex jijini Dar es salaam.

Kocha Hababuu ana hakika wachezaji wake watakamilisha azma ya ushindi katika mchezo huo wenye lengo ya kusaka nafasi ya kushiriki fainali za Afrika kwa vijana ambazo zitafanyika baadae mwaka huu nchini Niger.

Amesema pamoja na kuwa na mipango mizuri ya ushindani bado anaiheshimu timu ya vijana ya Afrika Kusini, kutokana na historia ya soka la nchi hiyo lakini bado akasisitiza kutokuwa na hofu yoyote kuelekea mchezo wa kesho.

Naye Kocha wa Afrika Kusini, Molefi Ntseki amerejesha kijembe kwa kusema anaziheshimu timu za Tanzania, na changamoto aliyonayo ni kuhakikisha anashinda mchezo wa dhidi ay Serengeti Boys, kutfuatia changamoto inayoikabili nchi yake ambayo kwa mara ya mwisho iliwasilishwa na timu ya vijana kwenye michuano ya Afrika miaka sita iliyopita.