KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, July 10, 2014

Simba na Mtibwa wang'aka mabadiliko ya tarehe ya kuanza kwa ligi kuu Tanzania bara

Kocha mkuu wa Simba Logarocic na msaidizi wake Matola
Uongozi wa vilabu vya vinavyo shiriki ligi kuu ya Soka Tanzania Bara vya Mtibwa Sukari na Simba SC vimesikitishwa na maamuzi yaliyochukuliwa na shirikisho la soka nchini TFF ya kusogeza mbele tarehe ya kuanza kwa ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa mwaka 2014-15.

Afisa habari wa klabu ya Mtibwa Sugar yenye maskani yake Manungu, Turiani mkoani Morogoro Thobias Kifaru amesema hatua hiyo ya TFF haikufuata nidhamu ya kiufundi na kimashindano hata kidogo na kwamba viongozi wa TFF walipaswa kufanya maamuzi hayo kwa kuwashirikisha viongozi wa klabu za ligi kuu, kwa ajili ya kupata muafaka wa pamoja.

Kifaru amesema  wakati kama huu wa maandalizi ya msimu mipango ya makocha wote huwa inaendana na Programu zao kwa mujibu wa kalenda huku pia suala la kiuchumi katika kuviweka vilabu hivyo kambini pia linaendana na kalenda hivyo kufanya maamuzi kama hayo ni kuharibu mipango hiyo kwa pamoja.
Amesema TFF wamekuwa wakifanya maamuzi kama hayo kila mara pasina kuzingatia hasara kubwa ambazo zimekua zikizikabili klabu za ligi kuu ambazo zinatumia kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya maandalizi.

Kikosi cha Mtibwa Sugar ya Morogoro
Kwa upande wa Wekundu wa Msimbazi Simba kupitia kwa afisa habari wake Asha Muhaji amesema licha ya kikosi chao kuanza mazoezi ya Gym hapo jana bado kusogezwa mbele kwa tarehe ya kuanza kwa ligi kuu kutoka Agosti 24 mpaka Septemba 20 kumewaathiri kwa kiasi fulani mipango yao ya maandalizi kwa ujumla kwa kuwa ratiba hiyo mpya inapangua mipango waliyokuwa wameiiwekea kabla ya kuanza rasmi kambi yao.

Muhaji amesema kuharibika kwa mipango hiyo kwa sasa, kunatoa changamoto mpya viongozi walioingia madarakani mwishoni mwa mwezi uliopita kujipanga tena na maandalizi yao kutegemeana na maoni ya mwalimu wao Mcroatia Zdravko Logarusic ambaye alikuwa akitarajiwa kurejea nchini hii leo.