KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, July 10, 2014

Waziri wa habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh Said Ally Mbaruk awataka TBL kupitia kinywaji cha Grand Malt kusalia sana Zanzibar

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Mhe. Said Ali Mbarouk akimkabidhi vifaa Afisa Michezo wa Mafunzo , Khamis Ali wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo vilivyotolewa na Grand Malt.(Picha na Haroub Hussein).
 Serikali ya mapinduzi Zanzibar imeiomba kampuni ya bia nchini TBL kupitia kinywaji cha Grand Malt kuendelea kuidhamini ligi kuu ya soka visiwani humo kwa lengo la kuendeleza dhana ya kutoa ajira kwa vijana kupitia medani ya soka.

Waziri wa habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh Said Ally Mbaruk amesema tangu TBL kupitia kinywaji cha Grand Malt walipokubalia kuidhamini ligi ya ZFA, kumekuwa na mabadiliko makubwa kwa vijana ambao kutokana na kuonyesha nia ya kutaka kujikita katika michezo hususana mchezo wa soka halia mbayo anaamini itaendelea kuisaidia serikali ya SMZ kutatua tatizo la ajira.

Said Ally Mbaruk amesema kampuni hiyo pia imeongeza chachu katika wigo wa kuundwa kwa timu ya taifa ya Tanzania ambapo kwa sasa wachezaji wengi wanaoitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars wanatoka visiwani Zanzibar.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Mhe. Said Ali Mbarouk akimkabidhi vifaa Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi , Issa Ahmada Jogoo wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo vilivyotolewa na Grand Malt.(Picha na Haroub Hussein).
Kwa msimu wa mwaka 2014-15 kampuni ya bia nchini TBL kupitia kinywaji cha Grand Malt imesaini mkataba wa kuidhamini ligi ya visiwani Zanzibar wa shilingi 244 tofauti na msimu uliopita ambapo kiasi cha fedha kilikuwa ni shilingi million 204.

No comments:

Post a Comment