KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, July 15, 2014

USAJILI KIANGAZI: SOUTHAMTON WAMTIA GUNDI RODRIGUEZ KWA MIAKA MITANO

Southampton tayari imesha mtia gundi Jay Rodriguez kwa miaka mingine mitano ingawa Liverpool walikuwa wakimtaka.
Southampton imetoa maelezo kuwa hatakuwa muhanga wa kuishiwa na wachezaji wote muhimu na wazuri na kwamba tayari imekamilisha kumsajili Jay Rodriguez kwa mkataba wa miaka zaidi mitano.
Tayari klabu hiyo imesha wapoteza wachezaji wake waliokuwa bora kikosini Luke Shaw aliyejiunga na Manchester United na Adam Lallana pamoja naye Rickie Lambert ambao wameelekea Liverpool lakini kwasasa wakijinasibu kuwa na nyota wengine baada ya kuondokewa na wachezaji wake hao.

Rodriguez bado ana miaka miwili ndani ya mkataba wake wa sasa tangu kujiunga nayo kwa mkataba wa miaka minne june June 2012.
Liverpool na Tottenham zote kwa pamoja zote zinavutiwa na mshambuliaji huyo lakini Southampton wameonelea kuw ni bora kusalia naye msimu ujao.
Rodriguez alifunga mabao 17 msimu uliopita na alikuwa katika mpango wa kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya England kilicho shiriki fainali za kombe la dunia kabla ya kuenguliwa katika dakika za mwisho kutokana na majeruhi ya mguu.

In training: Rickie Lambert has linked up with Brendan Rodgers' squad this week ahead of the season
Rickie Lambert yuko katika mpango wa Brendan Rodgers kuelekea msimu mpya.