|
Antionio Conte ameachana na kazi ya umeneja Juventus kwa hiari yake baada ya utumishi wake wa miaka minne ndani ya klabu hiyo. |
Antonio Conte amejiuzulu umeneja katika klabu yake ya Juventus kwa hiari yake baada ya utumishi wake wa miaka minne.
Meneja huyo mwenye umri wa miaka 44 ameondoka kwa kibibi kizee hicho cha Turin baada ya kuwaongoza kwa mfanikio na kutwaa mataja matatu mfululizo ya ligi kuu ya Italia maarufu kama Serie A.
Meneja huyo Mtaliano ambaye enzi za uchezaji wake mpira alikuwa ni nahodha wa kikosi cha Juventus, aliwahi kuiongoza na kufikia rekodi ya kufikisha alama 102 na kutwaa taji la 30 la Serial A.
Tanzazo hilo la kujiuzulu alilitoa kupitia mtandao wa klabu yake katika hali ya kushitua, wakati huu ambapo kigogo hicho cha Italia kikijiandaa kwa kampeni ya kuanza msimu mpya.
Zimekuwepo tetesi kuelekea mwishoni mwa msimu uliopita kuwa Conte alikuwa na mpango wa kuondoka, lakini baadaye alibadilisha mawazo.
Akiwa bado ana mwaka mmoja ndani ya mkataba wake na Juventus, Conte kupitia ujumbe wa video ambao aliutuma kupitia mtandao rasmi wa klabu hiyo amesema ameamua kujiuzulu kwa hiari yake.
Conte (wa pili kushoto) aliiongoza Juventus kushinda mataji matatu mfululizo ya Serie A na mataji mawili ya kombe la Italia
'Nimeamua kuutema mkataba wangu' Amesema.
'Nimepevuka kutoka na wakati na hisia zangu zimenituma nifanye maamuzi. Inawezekana ikawa ni ngumu kuendelea kushinda ukiwa na Juventus.
'Niwashukuru kwa yote mliyo nifanyia tangu nikiwa kama mchezaji na kama kocha. Siku zote nitakuwa karibu yenu, nataka kusema safari niliyo enda nayo hivi karibuni itakuwa historia.
'Kushinda ni ngumu. Kunakuja kwa juhudi kubwa, hususani katika klabu kama Juventus ambako kunashauku ya ushindi, lakini onyesha kuwa mimi mshindi.'
Taarifa zinasema kuwa kufuatia nafasi ya ukocha wa timu ya taifa ya Italia kuwa wazi kutokana na kujiuzulu kwa Cesare Prandelli
baada ya Azzurri kuondolewa katika hatua ya makundi ya fainali ya kombe la dunia nchini Brazil, Bado haijafahamika endapo Conte atajitupa kwenye kazi hiyo.
'Kwasasa nafikiria mambo ya wakati huu na kufanya maamuzi' Ameongeza.
Nahodha wa Juventus
Gianluigi Buffon amesema kuondoka kwa Conte ni msiba mkubwa kwani hakuna maelezo zaidi juu ya kuondoka kwake, lakini akasema kuondoka kwake hakuta athiri uwezo wa kikosi cha timu yao.
Mtengenezaji wa historia: Msimu wa mwisho wa Conte umuwezesha kuweka rekodi ya kufikia alama 102 katika ligi kuu ya Serie A
'Rais wa klabu Andrea Agnelli amemtakia kila la kheri Conte, na kumshukuru kwa yote aliyoyafanya Turin.
Ameandika kwenye mtandao wa klabu.
'Dear Antonio, umekuwa kiongozi mzuri na habari hizi zimenihuzunisha sana'
Sad: Juventus goalkeeper Gianluigi Buffon described Conte's exit as a 'serious loss' to the club
'Miaka mitatu pamoja umetuongoza kuweka historia ya mataji matatu mfululizo ya Serial A na mengine mawili ya Italian Cup.
'Umelifanya kundi hili kuwa na vipaji vya hali ya juu ambavyo vitamuwezesha kocha ajaye kuendelea kutengeneza mafanikio.
'Uko ndani ya rangi za kihistoria za mafanikio ya Bianconeri na kwa uchaguzi wowote ule ulichukua, ushindi wa Juventus utakufanya utabasamu popote.
'Antonio, tunakushukuru kwa kila jambi, mpaka milele'
Nahodha wa ukweli Conte (kushoto) ameichezea Juventus kwa zaidi ya michezo 500 kama mchezaji na kushinda mataji matano ya ligi.
Tayari bosi wa zamani wa Manchester City Roberto Mancini na meneja wa zamani wa AC Milan Massimiliano Allegri wameanza kuhusishwa na kazi hiyo Turin
Roberto Mancini tayari ameanza kuhusishwa kuchukua nafasi ya Conte
No comments:
Post a Comment