KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, July 16, 2014

LIVERPOOL WAANZA KUCHOKA SASA, SWANSEA CITY YAWAPIGA CHINI NA PAUNI ZAO MILIONI 8

Liverpool walikuwa wakimfuatiali mlinzi wa kushoto wa Swansea Ben Davies
Swansea imepiga chini ofa ya pauni milioni £8 za Liverpool kwa ajili ya kumsajili mlinzi wa kushoto wa Swansea Ben Davies.
Mlinzi huyo wa kimataifa wa Wales alikuwa katika mawindo makubwa  ya meneja Brendan Rodgers wa Liverpool ambaye amekuwa akisaka mlinzi wa kushoto ambapo mpango mwingine wa mlinzi wa kushoto wa Sevilla Alberto Moreno kuonekana kwenda mrama.
Sevilla ya Hispania wanahitaji pauni £18 ndipo wamtoe mlizni huyo, huku Liverpool wakiwa hawako tayari kulipa kiasi hicho. 
Rejected: But they had an £8m bid for him turned down
Pauni milioni £8 zimepigwa chini

Tottenham pia walimfuatilia kinda huyo mwenye umri wa miaka 21 kabla ya kuondoa nia yao hiyo kufuatia Swansea kumthaminisha kwa pauni milioni £12.
Davies alianza kuichezea Swansea mwaka 2012 kufuatia majeraha kumkumba Neil Taylor, na aliendelea kupiga soka mpaka akatimiza michezo 84 ya klabu hiyo katika misimu miwili iliyopita.
Alishinda League Cup akiwa chini ya Michael Laudrup katika msimu uliopita na kuichezea kwa michezo saba msimu uliopita katika michezo ya ligi ya Ulaya 'Europa League' kufuatia Swansea kufuzu kwa hatua ya timu 32 za mwisho.