Serengeti Boys tayari kuishambulia Afrika kusini Ijumaa uwanja wa Azam Comlex |
Afrika Kusini (Amajimbos) imewasili nchini kuikabili
Tanzania (Serengeti Boys) katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano
ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 itakayochezwa keshokutwa
(Julai 18 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Taarifa ya afisa habari na mawasiliano wa shirikisho la Soka nchini Tanzania TFF Bonface Wambura imesema timu hiyo yenye msafara wa watu 37 ilitua Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jana usiku (Julai 15 mwaka huu) na
imefikia hoteli ya Sapphire. Amajimbos itafanya mazoezi leo saa 10 jioni kwenye
Uwanja wa Azam Complex.
Waamuzi watakaochezesha mechi hiyo kutoka Shelisheli
wakiongozwa na Allister Barra tayari wamewasili nchini. Kamishna wa mechi hiyo
ni Andriamiasasoa Doda Nirimboavonjy kutoka Madagascar.
Makocha wa timu za Seregenti Boys na Amajimbos pamoja
na manahodha wao watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kesho (Julai 17
mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF).
Kiingilio katika mechi hiyo ni sh. 2,000. Tiketi
zitauzwa uwanjani katika magari maalumu siku ya mechi.
No comments:
Post a Comment