KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, July 16, 2014

Louis van Gaal amewasili jijini Manchester kesho kutambulishwa rasmi Carrington

Louis van Gaal amewasili jijini Manchester kabla ya kujichanganya na mazingira mapya ya kazi. Meneja huyo mpya wa Manchester United alitua jijini hapo kwa ndege binafsi na kutua majira ya saa mbili na dakika arubaini na kuelekea uwanja wa Carrington akiwa ndani ya Chevrolet nyeusi.

Atatambulishwa kwa wakuu wa klabu ya Manchester United ndani ya viunga vya mazoezi vya klabu hiyo na kutalii viunga hivyo vya klabu kabla ya kukutana na kikosi chake. 
Kocha huyo anatarajiwa kutambulishwa kwa waandishi wa habari hapo kesho.
Atua rasmi: Louis van Gaal (pichani nchini uholanzi mwishoni mwa wiki) awasili Manchester asubuhi ya leo.

Anatarajiwa kuondoka ijumaa akiwa na kikosi kizima caha kwanza kuelekea Marekani ambako watacheza michezo minne ya maandalizi ya kikosi.
Van Gaal atatambulishwa kwa kikosi Carrington kesho kabla ya kuanza mazoezi.