KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, July 16, 2014

MWINYI KAZIMOTO KUTUA DAR ES SALAAM KESHO KABLA YA MCHEZO DHIDI YA MOZAMBIQUE

Kikosi cha Stars kilichocheza mchezo dhidi ya Malawi ambao Stars iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lilifungwa na Amri Kiemba.
Washambuliaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wamewasili nchini leo asubuhi (Julai 16 mwaka huu) kutoka Tunisia kujiunga na Taifa Stars kwa ajili ya mechi dhidi ya Msumbiji itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mwinyi Kazimoto kutua kesho
Wachezaji hao wamefikia hoteli ya Courtyard, Seaview Upanga na leo (Julai 16 mwaka huu) watafanya mazoezi kwa programu maalumu waliyopewa na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij wakati wakiwasubiri wenzao.
Naye kiungo Mwinyi Kazimoto anayecheza mpira wa miguu katika klabu ya Almarhiya ya Qatar atawasili nchini kesho (Julai 17 mwaka huu) saa 1.30 asubuhi kwa ndege ya Qatar Airways.
Taifa Stars itawasili Dar es Salaam kesho (Julai 17 mwaka huu) saa 3.20 asubuhi kwa ndege ya Fastjet kutoka Mbeya tayari kwa maandalizi ya mwisho kabla ya kuivaa Msumbiji.