Imefahamika kuwa wachezaji watatu wa kigeni wa klabu ya Yanga kiungo Haruna Noyinzima na washambuliaji wawili wa kimataifa wa Uganda Hamisi Kiiza Diego na Emmanuel Okwi hatima yao ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake katika makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani iko mikononi mwa kocha mpya wa klabu hiyo Mbrazil Marcio Maximo.
Habari zilizoifikia rockersports kutoka kwa mmoja wa viongozi wa klabu hiyo ambaye hakutaka jina jina lake kutajwa mtandaoni humu, amesema ujio wa wachezaji wawili kutoka nchini Brazil mshambuliaji Geilson Santos Santana "Jaja" na Kiungo mshamabuliaji Andrey Marcel Ferreira Coutinho kunawaondoa mmoja wa wachezaji wa kigeni kutoka ukanda huu wa Afrika mashariki kwa kuwa wachezaji hao wa Brazil walioletwa na Maximo si wa majaribio bali wamekuja kufanya kazi.
Chanzo hicho kimesema kwa mujibu wa kanuni za usajili za shirikisho la soka nchini TFF ni dhahiri wachezaji wa kigeni wanatakiwa watano na mpaka sasa Yanga imefikisha idadi ya wachezaji saba hivyo basi kuna hatari kati ya Niyonzima na Okwi mmoja akaondoka Jangwani msimu huu.
Taarifa zaidi zinasema kumekuwepo na mazungumzo yanayo endelea baina ya wachezaji hao na kamati ya usajili ya klabu hiyo ambayo kimsingi yanagusa juu ya namna ya kumalizana nao huku zoezi hilo likikumbwa na presha kubwa kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment