Licha ya mafanikio ya kutwaa taji la kombe la dunia kwenye ardhi ya taifa lenye wendawazimu mkubwa wa soka dunia Brazil, Joachim Löw ameyaangazia macho yake kwa changamoto zijazo kwa lengo la kufika mbali zaidi kimafanikio kama ilivyokuwa kwa Uhispania kama Mabingwa wa Ulimwengu na Ulaya.
Kwasasa kocha huyo wa
 Ujerumani yuko mawindoni kumtafuta msaidizi wake mpya. 
Naibu kocha Hans-Dieter Flick, amekuwa msaidizi wa Löw tangu mwaka wa 
2006, wakati Löw alipoichukua mikoba kutoka kwa Jürgen Klinsmann baada 
ya kukamilika Kombe la Dunia lililoandaliwa katika ardhi ya nyumbani.
 Kuanzia Septemba mosi, Flick atachukua kazi ya mkurugenzi mkuu wa
 Shirikisho la Soka Ujerumani - DFB.
Mwezi wa Septemba utakuwa wenye shughuli nyingi kwa Die Mannschaft.
 Pembeni ya uteuzi huu, pia kutakuweko na mechi za kirafiki dhidi ya 
Argentina walioshindwa katika fainali, na Scotland.
Mnamo Oktoba 2013, Löw aliurefusha mkataba wake na Shirikisho la DFB 
hadi mwishoni mwa mashindano ya UEFA Euro 2016. Kocha huyo mwenye umri 
wa miaka 53 kisha atakuwa amekamilisha kipindi cha mwongo mmoja kama 
kocha wa Ujerumani.
Kocha wa zamani wa Mainz Thomas Tuchel anaripotiwa kuwa mmoja wa majina 
yanayotarajiwa kujaza pengo la naibu kocha wa taifa. Kocha huyo mwenye 
umri wa miaka 39 alihama klabu ya Mainz kwa ghafla mwishoni mwa msimu 
uliopita wa Bundesliga licha ya kuisaidia klabu hiyo kufuzu katika dimba
 la Europa League kwa mara ya pili katika historia ya klabu hiyo.
Rais wa DFB Niersbach ameweka wazi kuwa Löw atafanya uamuzi kamili 
kuhusiana na nafasi hiyo, na hapatakuwa na hali yoyote ya kuingilia kati
 kwa maafisa wengine wa DFB pamoja na wadau wa soka Ujerumani.
 

No comments:
Post a Comment