KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, July 18, 2014

Kocha Louis van Gaal wa Manchester United apeleka kikosi Marekani na kuwaacha wachezaji kibao akiwemo Evra, Fellaini

Kocha Louis van Gaal wa Manchester United
Kocha Louis van Gaal wa Manchester United ametangaza kikosi chake kitakacho kuwa safarini nchini Marekani kwa maandalizi ya kuanza msimu.
Wachezaji 25 ambao wameelekea Marekani mchana wa leo baada ya mazoezi mepesi uwanja wa Carrington mapema leo wakisheheni wachezaji wakiwemo wakonge kadhaa pamoja na wachezaji vijana. 
Bebe na Patrice Evra, wamekuwa wakihusishwa na kutaka kujiunga na Benfica na Juventus na hawakuwepo kwenye kikosi. Kiungo Mbrazil Anderson hatakuwepo katika msafara huo kufuatia kukumbwa mapema na dhahma ya majeruhi wakiwa mazoezini. 
 Dynamic duo: Wayne Rooney and Juan Mata (behind) have joined the squad after the World Cup
Wayne Rooney na Juan Mata yumo kikosini baada ya ushiriki wake katika fainali za kombe la dunia.
Wengine ambao hawakuwemo kikosini ni Javier Hernandez, Robin van Persie, Adnan Januzaj na Marouane Fellaini ambao wamepewa mapumziko baada ya fainali ya kombe la dunia nchini Brazil.
Michael Carrick hakusafiri kufuatia kufanyiwa upasuaji wa enka yake hapo jana na anatarajiwa kuendelea kuponya jeraha lake kwa miezi miwili.
Wachezaji wapya Ander Herrera na  Luke Shaw wenyewe wameelekea Marekani sambambsa na wakali Juan Mata na David de Gea.

Wachezaji 25 walioelekea Marekani kwenye kwa ziara ya Pre-season

Goalkeepers: David De Gea, Anders Lindegaard, Ben Amos, Sam Johnstone.

Defenders: Rafael, Jonny Evans, Chris Smalling, Phil Jones, Luke Shaw, Tyler Blackett, Michael Keane, Reece James.

Midfielders: Ander Herrera, Tom Cleverley, Darren Fletcher, Ashley Young, Wilfried Zaha, Shinji Kagawa, Juan Mata, Antonio Valencia, Nani, Jesse Lingard.

Forwards: Danny Welbeck, Wayne Rooney, Will Keane.

No comments:

Post a Comment