|  | 
| Nahodha Lahm wa Ujerumani Philipp Lahm | 
Baada ya kurudi nyumbani na Kombe la Dunia mikononi mwake, nahodha wa 
timu ya taifa ya Ujerumani Philipp Lahm amestaafu kutoka soka la 
kimataifa. Hayo yamethibitishwa na Shirikisho la Soka Ujerumani – DFB 
Beki huyo wa Bayern Munich mwenye umri wa miaka 30 amefanya uamuzi huo, baada ya kumpigia simu rais wa DFB Wolfgang Niersbach.
Niersbach alimshukuru kwa mchango wake wa miaka kumi katika timu ya 
Ujerumani ambapo pia aliibuka kuwa kielelezo kwa chipukizi wengine. 
Kushinda Kombe la Dunia ni kama kilele cha kazi yake ya kandanda kufikia
 sasa, ambayo inajumuisha pia taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, mataji 
sita ya Bundesliga na sita ya Kombe la Shirikisho la Soka Ujerumani.
Lahm alianza kazi yake ya kandanda mnamo Februari 2004 katika ushindi 
wao wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Croatia. Kisha akaichezea 
Ujerumani mechi 113 na kufunga magoli matano. Kabla ya kushinda Kombe la
 Dunia la 2014, Lahm na timu yake waliibuka washindi wa tatu Kombe la 
Dunia mwaka wa 2006 na 2010, na wakawa makamu bingwa wa dimba la Euro 
2008. Pia alicheza katika Euro 2004 na 2012.
Mkataba wa Lahm na mabingwa wa Bundesliga Bayern ulirefushwa kabla ya Kombe la Dunia na utakamilika mwaka wa 2018.
 
No comments:
Post a Comment