KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, August 23, 2014

Angel Di Maria na Marcos Rojo wateta kuhusu Manchester United wakati harufu ya Di Maria ikinukia Old Trafford

Angel Di Maria azungumza na Mu-Arjentina mwenzake Rojo na kusema huenda wakaungana Old Trafford
Taarifa zinasema kuwa Angel Di Maria ameongea na nyota mpya wa Manchester United Marcos Rojo na kwamba anataka kuungana naye Old Trafford kabla ya msimu wa uhamisho wa kiangazi hii haujafungwa rasmi.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Argentina amekuwa akihusishwa sana na kuondoka Real Madrid, huku bosi Carlo Ancelotti akithibitisha kuwa rasmi ameshapokea maombi ya uhamisho huo wake.

Vilabu vyote Manchester United na Paris Saint-Germain wamekuwa wakipigana vikumbi kusaka saini yake huku Barcelona wakiaminika kuwa tayari wameshawasilisha ombi hilo.

Lakini wakati Real wanaonekana kutokuwa tayari kuwauzia wapinzani wao wakubwa, na wakati PSG wakijiondoa katika mpango huo basi wazi kuwa Di Maria atakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuelekea Old Trafford.
 
Kwa mujibu wa redio Marca,ya nchini Hispania ni kwamba winga huyo wamekuwa katika mawasiliano na mwenzake katika kikosi cha timu ya taifa ya Argentina Rojo wakijadili juu ya mpango wake huo wakati huu ambapo Rojo akiwa amesha tua katika kikosi cha Louis van Gaal.