KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, August 24, 2014

Mshambuliaji wa JS Kabylie Ebosse afariki dunia kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali nchini Algeria

Aliyekuwa Mshambuliaji wa JS Kabylie Albert Ebosse aliyefariki dunia kutokana na kurushiwa mawe na mashabi
Mchezaji mpira kutoka Cameroon amekufa baada ya kupigwa kichwani wakati mashabiki waliokereka waliporusha mawe mwisho wa mechi ya ligi ya Algeria.

Albert Ebosse, aliyekuwa na umri wa miaka 24, ndiye aliyetia magoli mengi kabisa katika ligi ya Algeria msimu uliopita.

Alirushiwa kitu wakati mashabiki walipokerwa kuwa timu yake, JS Kabylie, iliposhindwa kwa magoli mawili kwa moja katika mechi iliyochezwa nyumbani, Tizi Ouzou.
Yeye ndiye aliyepata hilo goli moja kwa timu yake.

Tukio hilo limetokea baada ya Ebosse kuifungia timu yake katika mchezo ambao JS Kabylie wakikubali kufungwa uwanja wa nyumbani bao 2-1 na USM Alger hapo jana Jumamosi.

Ebisse aliyekuwa na umri wa miaka 24 alikimbizwa hospitali huko Tizi Ouzou, mashariki ya jiji la Algiers, baada ya mashabiki kurusha mawe kwa wachezaji wakati wakirejea katika vyumba vya kubadilishia nguo baada ya mchezo kumalizika.

Ebosse alitangazwa kuwa amefariki dunia kutokana na jeraha kubwa alilopata

Wizara ya mambo ya nchi ya Algeria imeamrisha uchunguzi ufanywe.
Ligi ya Algeria imefunga uwanja wa mpira wa timu ya JS Kabylie na imeitisha mkutano wa dharura Jumatatu.