KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, August 13, 2014

KOLO TOURE AGOMA KUELEKEA UTURUKI

Mlinzi wa kimataifa wa Ivory Coast Kolo Toure, anasema haondoki Liverpool ng'o
Mlinzi wa kimataifa wa Ivory Coast Kolo Toure amepiga chini mpango wa kuelekea nchini Uturuki na kutangaza nia yake ya kuendelea kusalia Liverpool.
Mlinzi huyo wa kati aliwasili Anfield mwaka uliopita akitokea Manchester City na taarifa za tetesi za hivi karibu zikisema huenda angeondoka klabu hapo tangu kusajili kwa Dejan Lovren kwa ada ya pauni milioni £20 akitokea Southampton.
Toure hakuwa na msimu  uliopita kufuatia kufanya makosa kadhaa mzurikatika michezo dhidi ya Hull City, West Brom na Fulham.
Baadhi ya mashabiki wamekuwa wakimlaumu kwa aina ya ulinzi wake.