KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, August 12, 2014

Mashabiki wa LIverpool hawamtaki Eto'o

Mshabiki wa Liverpool hawafurahishwi na taarifa za kusajiliwa kwa Samuel Eto’o Anfield
Mashabiki wa LIverpool wameanza kuonyesha hasira zao kupitia mitandao ya kijamii baada ya taarifa za kwamba huenda mshambuliaji Samuel Eto’o akasajili wa na klabu yao.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea ameripotiwa kuwa katika mazungumzo na wekundu hao wakati huu ambapo meneja Brendan Rodgers anatafuta mshambuliaji kwa ajili ya msimu mpya ambaye atachukua nafasi ya Luis Suarez aliyeuzwa kwa Barcelona.