KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, August 12, 2014

Liverpool kumkosa mlinzi wa kushoto wa Sevilla Moreno kisa mkwanja mdogo

Alberto Moreno
Shauku ya Liverpool ya kumsajili Alberto Moreno inaonekana kukwaa kisiki kufuatia klabu ya Sevilla kuwaonya wekundu hao kuwa hawatakubali ofa yoyote chini ya kiwango cha ada waliyoitangaza wao Sevilla.
Moreno alitarajiwa kucheza mchezo wake wa mwisho katika kikosi cha Sevilla usiku huu ukiwa ni mchezo michuano ya Uefa Super Cup dhidi ya Real Madrid mchezo ambao unatarajiwa kupigwa 'Cardiff City Stadium', wakati huu ambapo mpango wa kuelekea Anfield ukionekana kukwama.
Lakini inavyoonekana ni kwamba bado Sevilla hawajaridhika na ofa ya juu ya Liverpool ya kumnunua mlinzi huyo wa kushoto.
‘Kumekuwepo na mazungumzo juu ya Moreno karibu siku 8 mpaka 10 zilizopita lakini bado kufikiwa makubaliano’ ananukuliwa Rais wa Sevilla Jose Castro.
‘kama ofa ya Liverpool itakuwa ya kuvutia ataondoka. Kama haitakuwa hivyo atasalia na hakuwa kitakacho tokea kabisa.’
Mabingwa hao wa Europa League wa Ulaya inaarifiwa kuwa wanataka kiasi cha pauni milioni £20 ndipo wamuuze mlizni huyo mwenye umri wa miaka 22, lakini Liverpool wanaonekana kukwama wakiwa na kiasi cha pauni milioni £16.