KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, August 12, 2014

Rihanna kuweka ofa mezani kuinunua Liverpool ushauri kutoka kwa Drogba

Rihanna anajipanga kuonyesha mapenzi yake mapya katika mchezo wa mpira ambapo sasa ana elekea kuzindua mpango mpya kuinunua klabu ya Liverpool. 

Malkia huyo wa muziki wa Pop aliteka nyoyo za watu katika kombe la dunia nchini Brazil, alipokuwa akionekana kuchanganywa na matukio ya michezo ya fainali hizo.

Taarifa zinasema kuwa msanii huyu amekuwa akitaka kuwekeza katika klabu ya nchini England huku gazeti la El Mundo Deportivo likiarifu kuwa Liverpool ndio chaguo lake.

Gazeti hilo limearifu kuwa Rihanna ameshauriwa na rafiki yake wa karibu ambaye ni mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba kuweka ofa yake Anfield.
Huyu ni Rihanna akichizika na soka .