KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, August 11, 2014

Breaking news: Didier Drogba sasa kuikosa ligi kuu ya England kwa miezi nne mpaka sita

Didier Drogba akigumia maumivu
Didier Drogba huenda asirudi uwanjani katika kipindi cha miezi minne mpaka sita kufuatia jeraha la kifundo alilolipata wakati wa mchezo wa maandalizi ya msimu dhidi ya Ferencvaros Jumapili iliyopita.

Mshambuliaji huyo wa 'The Blues' amekumbwa na jeraha hilo wakati akishuka chini kutoka hewani akipiga mpira kichwa dakika ya 28 mchezo ambao Chelsea ilishinda 2-1 huko Groupama Arena mjini Budapest.

Huu ni mfano wa jeraha la Drogba
Gazeti la Marca la nchini Hispania limedai kuwa jeraha la Drogba linaweza kuwa baya zaidi ya hapo awali kwani vipimo vinaonyeshwa kuwa mifupa inayounganisha kikanyagio na kisigino imeachana.