KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, August 11, 2014

Jose Mourinho amemwambia Sami Khedira asubiri amalizie mkataba wake na Real Madrid ali aweze kutua Chelsea

Sami Khedira
Nyota anayewindwa na Arsenal Sami Khedira ameambiwa kuwa anapaswa kusahau habari  za washika mitutu na asubiri uhamisho huru wa kiangazi ijayo atakapo jiunga na Chelsea hii ikiwa ni kauli ya Jose Mourinho.

Nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani amekuwa akifukuziwa msimu wote huu wa kiangazi na Arsenal, hizi zikiwa ni taarifa ambazo zimekuwa zikiendelea kuchukua nafasi sehemu kubwa ya msimu huu wa uhamisho wa kiangazi, ingawaje bosi wa washika mitutu Arsene Wenger anaonekana kuwa mbali na mafanikio ya kumsajili.

Lakini wakati harakati za kuelekea Emirates zikionekana kukwama ,Mourinho sasa anaonekana kujitupa katika varangati hilo na taarifa zinasema kuwa Mourinho alimwambia Khedira asubiri msimu ujao ili ajiunge na Chelsea.

Kiungo huyo amesaliwa na mwaka mmoja wa mkataba wake akiwa na Real Madrid.