KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, August 28, 2014

ROCKERSPORTS AUDIO: Kama hukupata nafasi ya kumsikia Okwi na Hans Poppe wakati akisajili Simba, basi sikiliza hapa

Okwi akiwa karibu na mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Zackaria Hans Poppe
Kamati ya usajili ya klabu Simba imetangaza kumsajili mshambuliaji wao wa zamani Emmanuel Okwi ambaye msimu uliopita alikuwa kwa mahasimu wao wa soka Yanga.

Akiongea hii leo mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo Zackaria Hans Poppe amesema wamemsajili Okwi baada ya mshambuliaji huyo raia wa Uganga kuomba kusajiliwa na klabu hiyo kufuatia kuvunjiwa mkataba na Yanga.

Poppe amesema mkataba wa Okwi na Simba ni wa wazi kwani mchezaji huyo ambaye amejiunga na Simba akiwa huru atakuwa huru kuondoka muda wowote atakapo taka kufanya hivyo.

Bofya Sauti ya Hans Poppe akiongea na waandishi wa habari kuhusu usajili wa Okwi


Kwa upande wake Okwi amewataka wapenzi wa Simba kumchukuliwa yeye kama mchezaji mpya kwao na kwamba wasahau yaliyopita na wampokee kama mchezaji kijana mpya kwao

Bofya sauti ya Okwi akiongelea usajili wake Simba

Kabla ya kujiunga na Yanga Okwi alikuwa akiichezea Sports Club Villa ya Uganda ambayo alijiunga nayo alitokea Etoile Du Sahel ya Tunisia ambako Okwi aliikimbia klabu hiyo kutokana na kile kilicho daiwa kuwa alinyimwa mshahara wake kwa zaidi ya miezi kinyume na makubalino ya mkataba.

Okwi anasajiliwa na Simba ikiwa siku mbili zimesalia kabla ya dirisha la usajili wa wachezaji wa ndani halijafungwa huku usajili wa wachezaji kutoka nje dirisha lake likitarajiwa kufungwa Septemba 6 2014

No comments:

Post a Comment