KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, September 16, 2014

Guardiola anaamini kuwa kushindwa kwa Manchester United kutinga ligi ya mabingwa Ulaya ni somo kwa timu kubwa Ulaya

Guardiola anaamini kuwa kushindwa kwa Manchester United kutinga ligi ya mabingwa Ulaya ni somo kwa timu kubwa Ulaya

Bosi wa Bayern Munich Pep Guardiola amesema kuanguka kwa kigogo cha soka duniani klabu ya Manchester United kutoka katika zama za mafanikio ni onyo kwa vilabu vingine vikubwa barani Ulaya na kutanabaisha kuwa klabu hiyo yenye maskani yake Old Trafford haikuwa na nguvu ya kutosha kuwasajili wachezaji wake katika kipindi cha usajili cha majira ya kiangazi.
United imeshindwa kutinga katika ligi ya vilabu bingwa barani Ulaya jambo ambalo limekuwa ni mshituko mkubwa kote barani humo na Guardiola anaamini kuwa hakuna klabu yoyote kubwa itakayoweza mbele yao kama ilivyokuwa kwa United.
“Sisi ni timu isiyofungika na tuko imara bahati mbaya kwao hawapo katika ligi ya mabingwa pengine msimu ujao" amesema bosi huyo wa zamani wa Barcelona.
Van Persi wa Manchester United atakuwa mtazamaji wa ligi ya mabingwa Ulaya
‘Hivi ndivyo ilivyo katika mchezo wa mpira wa miguu, ni mchezo wa ajabu.
‘Kila wiki unapaswa kuwa tayari, kila wiki unapaswa kuwa tayari.’
Guardiola pia amethibitisha kuwa Louis van Gaal alijaribu kuwasajili wachezaji wake Arjen Robben, Bastian Schweinsteiger na Thomas Mueller kiangazi yote lakini United walishindwa kumudu hilo.
‘Hawakuwa na pesa ya kutosha kumsajili mchezaji huyo'.

No comments:

Post a Comment