KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, September 16, 2014

Luis Gustavo anasema si Arsenal wala klabu nyingine yoyote itakayomfanya kuondoka Wolfsburg

Luis Gustavo amesisitiza kuwa hataihama Wolfsburg
Luiz Gustavo anasisitiza kuwa hakuwahi kuwa na wazo la kuihama Wolfsburg akiondoa tetesi kuwa alikuwa na mpango wa kujiunga na Arsenal.
The Gunners waliripotiwa wakimtaka kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil wakati wa dirisha la usajili la kiangazi lakini kufuatia mpango huo wa Arsenal kuginga mwamba tetesi zikaendelea kusema kuwa mpango huo wa uhamisho umehamishiwa mwezi Januari.
Hata hivyo , Gustavo anasisitiza kuwa hana mpango wa kujiunga wa kuihama Wolfsburg, hata kama kitatokea klabu nyingine inamtaka.
‘Nina furaha sana hapa VfL Wolfsburg ni klabu kubwa kuichezea na napendelea maisha ya Ujerumani na fikra za kijerumani,’ Alikuwa akiongea na gazeti la Bild.
‘nafikiria hatma yangu ya baadaye bado iko hapa na nadhani kuendelea kucheza hapa kwa miaka mingi kwasababu ninalielewa jiji la Wolfsburg.

No comments:

Post a Comment