KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, September 17, 2014

MBINU MBOVU ZA MENEJA WENGER ZINAZAA KIWANGO KIBOVU KWA ARSENAL, MESUT OZIL NI MCHOVU?

Wenger unawachosha mashabiki wa Arsenal
Kichapo cha Usiku jana kuamkia leo kutoka kwa Borussia Dortmund kilikuwa ni ni moja kati ya usiku wa aibu kwa mashabiki wa Arsenal.

kupitia kurasa za kijamii wapenzi wa timu hiyo walionyesha hasira zao lakini ukirudi upande wa pili ni dhahiri kuwa imekuwa ni jambo la kawaida kwa Arsenal kuwa mwenendo huo hasa inapokuwa inacheza katika uwanja wa ugenini hususani dhidi ya timu kubwa.

Ni dhahiri kuwa mashabiki wa Arsenal wana hofu kubwa ya kuelekea kwenye taji la Ulaya kwa mbinu hizi zilizo pitwa na wakati za uchezaji.

Katika mchezo dhidi ya Manchester City kulikuwa na kiwango cha kutia moyo, lakini katika mchezo mkubwa wa mabingwa Ulaya hapo jana kuna hali ya kuogopesha kutokana na mfumo wa uchezaji.

Bosi wa Dormund Jurgen Klopp alimtoa kabisa katika njia bosi wa Arsenal Arsen Wenger.

Aina ya Kikosi ambacho Wenger amekitumia kilikuwa nje ya kiwango kabisa akiwatumia wachezaji kama Aaron Ramsey na Mesut Ozil wakati kuna Alex Oxlade-Chamberlain na Santi Cazorla wakifuatilia mchezo kutoka katika benchi kitu ambacho kiliwachanganya wengi.

Oxlade-Chamberlain alipoingia alibadilisha mchezo kiasi kuwafanya Dortmund kuanza kuvuruga aina ya mchezo wao na sura ya mchezo kubadilika huku nguvu na majukumu yake yakionekana kuvutia.
Wenger anamtumia mjerumani Mesut Ozil hata kama hayuko fomu
Wenger alikuwa na wachezaji wengi sehemu ya kiungo lakini mchezaji anapokuwa nje ya kiwango ana kawaida ya kumtumia mpaka anarejea tena katika kiwango chake. Swali ni ujumbe gani anapeleka mwa wachezaji wa akiba?

Ozil ni mchezaji bora katika kikosi cha Arsenal. Kujenga ubora wa kikosi hata kama hayupo unapaswa kujenga ubora kwa wengine walioko kikosini, vinginevyo ni kulazimisha kumtumia hata kama kiwango chake kinaangusha uwezo wa kiushindani.

Ni wazi inauma kumuona nyota huyu wa kimataifa wa Ujerumani kutokuonyesha juhudi katika baadhi ya michezo lakini hapa wakulaumiwa ni yeye mwenyewe meneja Wenger kwa kiwango kibovu cha kikosi chake na si Ozil. Ina shangaza kumuona mchezaji huyo katika winga ya kikosi kila mchezo.

Hiki ni kitu kingine ambacho Wenger atawakera mashabiki wa timu ya Arsenal ni wazi atamtumia Ozil winga ya kushoto mchezo wa jumamosi na huenda akaendelea kutumia kikosi kile kile cha kwanza kilichocheza dhidi ya Dortmund.

Mfumo haufanyi kazi lakini ana ung'ang'ania. Wachezaji wanacheza hovyo ana endelea kuwatumia hao hao. Meneja anakera kipindi hiki, inachukiza kuangalia timu ikicheza.