KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, September 7, 2014

PHIRI AANZA KUONYESHA MAKUCHA SIMBA, YAICHAPA GOR MAHIA 3-0

Wachezaji wa Simba wakishangilia moja ya mabao ya timu hiyo jana
Mshambuliaji Emmanuel Okwi (kushoto) wa Simba akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Gor Mahia katika mechi ya jana.
SIMBA jana iliichapa Gor Mahia ya Kenya mabao 3-0 katika mechi ya kirafiki ya kimataifa ya soka iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mechi hiyo, Simba ilimchezesha kwa mara ya kwanza mshambuliaji wake nyota kutoka Uganda, Emmanuel Okwi, baada ya kumsajili kutoka kwa wapinzani wao wa jadi, Yanga.

Okwi, alijikuta akiwa kwenye wakati mgumu kutokana na mashabiki wa Yanga kumzomea kila alipogusa mpira.

Mshambuliaji Paul Kihongera kutoka Kenya, aliibuka shujaa wa Simba baada ya kuifungia mabao mawili kati ya matatu. Bao lingine lilifungwa na Ramadhani Singano 'Messi'.

Wakati huo huo, Yanga inashuka dimbani leo kumenyana na Big Bullets ya Malawi katika mechi ya kirafiki itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mechi hiyo itakuwa ya pili ya kimataifa kwa Yanga, kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania Bara, ikiwa chini ya Kocha mpya, Marcio Maximo kutoka Brazil.