Shirikisho la kandanda Uingereza, FA, limechapisha mpango unaonuia
kupunguza wachezaji wasio wa asili ya muungano wa Ulaya (EU) wanaochezea
taifa hilo kwa kiasi kinachoweza kufika asilimia 50.
Watawala hao wa soka Uingereza wamechora orodha ya mabadiliko kwa
muundo wa sasa katika harakati za kuongeza idadi na ubora wa talanta
asili katika nchi hiyo.
Orodha hiyo imewasilishwa kwa ligi ya Premier, ligi ya Kandanda na
muungano wa wachezaji na mameneja na nia ya kuanza kuitekeleza kabla ya
mwanzo wa musimu wa 2015-16.
FA wanashikilia mpango huo utawezesha taifa lao kubobea kwenye Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar.
No comments:
Post a Comment