KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, September 18, 2014

ZINEDINE ZIDANE KUFUNGIWA MIEZI SITA, PATA MKASA KAMILI............

Kocha wa Real Madrid B Zinedine Zidane huedna akakabiliwa na kifungo cha kusimama kufundisha soka kwa miezi endapo atakutwa na hati ya kuongoza benchi la ufundi bila ya kuwa na leseni halali
Zinedine Zidane huenda akafungiwa kufundisha soka kwa miezi sita endapo atakutwa na makosa ya kuifundisha kikosi cha pili cha Real Madrid bila ya leseni halali.
Chama cha kitaifa cha makocha nchini Hispania CENAFE kimemshitaki nyota huyo wa zamani wa dunia ikiwa ni mwanzoni tu mwa msimu na sasa kamati ya mashindano ya nchi hiyo inaangalia uwezekano wa kama Real Madrid imevunja sheria nambari 104 ya kanuni zake ambayo inaweza kumfungia kati ya michezo minne na 16 au miezi sita.
Kikosi B cha Real Madrid kinatambulika kama 'Castilla' kimedai kuwa namba moja wa kikosi hicho ni Sergio Sanchez na kwamba Zidane ni kocha wa pili.
Hata hivyo wanaomshutumu mfaransa huyo wamewasilisha ushahidi na vielelezo vya maandishi na mkanda wa video kwamba hilo si shauri la kujadiliwa na kwamba nyota huyo wa zamani wa Real Madrid ni kweli anafanya kazi ya ukocha namba moja wa kikosi B.
Zidane attends the Predator Arena tournament in Arles, Southern France earlier this week
Zidane alikuwepo katika michuano ya Predator Arena huko Arles, kusini mwa nchi ya Ufaransa mapema wiki hii

Kocha namba moja nchini Ufaransa anatakiwa kuwa na diploma ya ngazi ya tatu ambapo Zidane, ambaye wiki hii ameweka wazi kuwa anataka kuwa kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa siku moja bado hajapata sifa hiyo.
Timu ya Madrid B katika miaka ya hivi karibuni imekuwa na matokeo mabaya wakimaliza katika nafasi ya tatu kutoka chini katika kundi la pili la ligi daraja la pili B ikifungwa michezo mitatu kati ya minne ya michezo yao waliyocheza.
Rais wa CENAFE, Miguel Galán, chombo ambacho kimemlalamikia amesema
'Real Madrid ni moja kati ya taasisi kubwa ya michezo inayotambuka duniani na alama ya michezo, lakini inapaswa kufuata sheria zilezile tulizojiwekea kama ilivyo kwa mtu mwingine yoyote  vingine mashindano yanakosa usawa'
Zidane (left) was Real Madrid manager Carlo Ancelotti's assistant during the 2013-14 season
Zidane (kushoto) alikuwa msaidizi wa meneja wa Real Madrid manager Carlo Ancelotti msimu wa 2013-14