KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, September 18, 2014

HIvi unajua ni vipi Mourinho alivyomkosa mlinzi Rafael Varane wa Real Madrid, kisa kizima hiki hapa.............

Rafael Varane
Chelsea ilikuwa katika kibarua pevu cha kusaka saini ya mlinzi kinda wa Real Madrid Rafael Varane kabla ya Madrid kuikata maini kwa kutangaza kufunga naye mkataba mwingine wa miaka sita.
The Blues walikuwa wakihusishwa na kumtaka dogo huyo mwenye umri wa miaka 21 karibu kiangazi yote huku bosi wa Madrid Jose Mourinho akihusishwa na mchezaji huyo ambapo alinukuliwa akimsifia kama ilivyo mbinu yake kubwa ya kunasa nyota wakubwa ambapo alikaririwa akisema ‘the best young defender in the world(mchezaji bora anayechipukia kuliko wote duniani)’.
Lakini Real Madrid wakamzodoa baada ya Varane kuanguka saini ya kusalia Bernabeu kwa miaka mingine sita ijayo mpaka 2020.
Madrid ilitangaza kupitia tovuti yake kuwa ‘The Real Madrid CF inatangaza kuongeza mkataba na mchezaji wake Raphael Varane mpaka June 30, 2020.’Hahahahaaaa ikawa ndio basi tena.

No comments:

Post a Comment