KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, September 18, 2014

Kumekucha vodacom League: Yanga kuifuata Mtibwa sugar bila ya Coutinho na Tegete

Washindi wa Ngao ya Jamii msimu wa 2014/2015 timu ya Young Africans kesho asubuhi wanatarajia kuondoka jijini Dar es salaam kuelekea mjini Morogoro tayari kwa mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya wakata miwa Mtibwa Sugar katika dimba la Uwanja Jamhuri.

Kikosi cha Young Africans kimekua kikiendelea na mazoezi kila siku tangu tangu baada ya mchezo wa jumapili, ambapo kocha mkuu Marcio Maximo amekua akiwanoa vijana wake kuhakikisha wanakua fit kwa mchezo huo wa jumamosi.

Young Africans chini ya mbrazil Marcio Maximo imepania kuhakaikisha safari hii inavunja mwiko wa kukosa ushindi katika dimba la Jamhuri kwa takribani miaka minne mfululizo, na maandalizi ya mchezo yanakwenda vizuri kuhakikisha kikosi kinaibuka na pointi tatu muhimu.

Kocha Mkuu Marcio Maximo mara baada ya mazoezi ya leo katika shule ya Sekondari Loyola, amesema vijana wake wote fit kwa mchezo huo na kikosi kinatarajia kuondoka asubuhi ili vijana waweze kupata muda mzuri wa kupumzika.

Aidha Maximo amesema anatambua Mtibwa Sugar wana kikosi kizuri ambacho kimekaa pamoja kwa muda mrefu, baadhi ya wachezaji aliwahi kuwafundisha akiwa kocha wa timu ya Taifa (Taifa Stars) ikiwa ni pamoja na kocha wao Mecky Mexime.

 "Sisi tumejiandaa kuhakikisha tunapata ushindi katika mchezo wa jumamosi, natambua utakua ni mgumu sababu Mtibwa watakua nyumbani wakihitaji pointi tatu muhimu lakini hata sisi tunakwenda Morogoro kuhakikisha tunapata pointi tatu pia "alisema Maximo.

Kuhusu maendeleo ya mchezaji Andrey Coutinho na Jerson Tegete wanaendelea vizuri na mazoezi lakini daktari ameona wabakie jijini Dar es salaam wakiendelea na programu nyingine chini ya usimamizi wa madaktari na wataungana na kikosi kitakaporejea jijini kwa mazoezi ya pamoja.

Wachezaji wanaotarajia kusafiri kesho kuelekea Morogoro ni:
Makipa: Deo Munishi "Dida", Juma Kaseja na Ally Mustafa "Barthez"
Walinzi: Juma Abdul, Oscar Joshua, Rajab Zahir, Kelvin Yondani na Nadir Haroub "Cannavaro"
Viungo: Mbuyu Twite, Omega Seme, Hassan Dilunga, Nizar Khalfani, Haruna Niyonzima na Said Juma "Makapu"
Washambuliaji: Said Bahanuzi, Hussein Javu, Hamis Kizza, Geilson Santos "Jaja", Saimon Msuva na Mrisho Ngasa

No comments:

Post a Comment