KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, September 18, 2014

Suso wa Liverpool kujiunga na AC Milan mwezi Januari

Nyota kinda wa Liverpool  Suso ameripotiwa kukubali kujiunga na kigogo cha soka nchini Italia AC Milan kwa uhamisho wa kudumu huku swali likisalia kuwa ni lini mchezaji huyo mhispania kijana ataelekea Rossoneri.
Suso, ambaye amekuwa katika kikosi cha kwanza cha Liverpool mara 14 alijiunga Anfield mwaka 2010, amekubali kuingia kandarasi ya miaka minne mkataba wenye thamani ya pauni £1.2 kwa mwaka hii ikiwa ni kwa mujibu wa habari kutoka nchini Italia.
Kijana huyu raia wa Hispania amekuwa mchezaji huru tangu kumalizika kwa mkataba msimu uliopita huku taarifa zaidi zikisema kuwa Milan wanajipanga kukamilisha usajiliwa kiungo huyo mshambuliaji mwezi Januari.