KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, September 11, 2014

YANGA NA FC LUPOPO KUKUTANA FIFA JUU YA FEDHA ZA MKOPO ZA MBUYU TWITE( Msikilize katibu wa FC Lupopo hapa)

Mbuyu Twite akitia dole gumba mbele ya Abdalah Bin Kleb

Katibu mkuu wa klabu ya FC Lupopo ya nchini Congo yuko nchini Tanzania kwa lengo la kufuatilia malipo ya pesa za mkopo za mlinzi Mbuyu Twitte ambaye ameongeza mkataba wa mwaka mmoja na klabu yake ya Yanga kufuatia mkataba wake wa awali wa misimu miwili kumalizika.

Akiongea na Rockersports katika mahojiano maalum, katibu mkuu wa FC Lupopo aliyejitambulisha kwa jina la Constantine Kabika amesema klabu yake ya Lupopo iliingia makubalino na Yanga ya kumsajili Mbuyu kwa mkopo wa miaka miwili na kwamba kipindi hicho cha makubaliano ya mkopo tayari kimemalizika.

Kabika amesema FC lupopo imekuwa katika mawasilino na Abdalah Bin Kleb na Seif Abdalah (maarufu Seif Magari) ambao hapo kabla wakiwa katika kamati ya usajili ya Yanga ndio waliomsajili mchezaji huyo akitokea katika klabu ya APR ya Rwanda lakini amekuwa akizungushwa juu ya suala hilo na kwamba sasa FC Lupopo imeanza kuchukua hatua nyingine za kuishitaki klabu hiyo shirikisho la soka nchini TFF na shirikisho la soka duniani FIFA.
Mbuyu Twite pamoja na Haruna Niyonzima enzi hizo wakiichezea APR ya Rwanda kabla ya kujiunga na Yanga

Amesema ameshangazwa na viongozi hao kutaka kumpa yeye kama katibu kiasi cha dola elfu tano ambazo yeye binafsi hakujua ni za nini kwakuwa makubalino ni baina ya vilabu viwili ambavyo vilikubaliana malipo ya mchezaji huyo kuwa dola elfu ishirini na mkataba baina ya vilabu hivyo upo TFF na kwamba aliyekuwa mkurugenzi wa mashindano wa TFF Saad Kawemba alishuhudia makubaliano hayo.

Katibu huyo wa Lupopo fc, Kabisa amesema kinachomshangaza zaidi ni kuwa hata baada ya mkataba huo kumalizika, bado Yanga imeendelea kumsajili mlinzi huyo bila ya mawasiliano yoyote na Lupopo fc ambao kimsingi ni mchezaji wao halali na kwamba walikubaliana wawasiliane baada ya mkataba huo kumalizika endapo Yanga ingependa kuendelea kuwa naye, jambo ambalo Yanga imeshindwa kutekeleza ilhali Mbuyu si mchezaji wa Yanga tena.

Amesema amekuwa akifanya mawasiliano na mlinzi huyo ambaye kwasasa amekuwa haonyeshi ushirikiano na yeye, huku habari za chini ya kapeti alizonazo ni kuwa tayari Yanga imempatia kiasi cha dola elfu moja na mia tano za kwake kama mchezaji na kumsainisha mkataba wa mwaka mmoja, huku wao Lupopo fc wakiendelea kusumbuliwa na uongozi wa Yanga kupitia kwa wajumbe wa zamani wa kamati ya Usajili Bin Kleb na Seif Magari.


Kabika amefunguka zaidi kwa kusema FC Lupopo ina mkataba wa miaka minne na Mbuyu Twite ambao utamalizika baada ya msimu huu na kwamba APR ya Rwanda ilimuuza kimakosa mlinzi huyo kwa Yanga kwani wakati wanamuuza alikuwa ndio kwanza ana mwaka mmoja ndani ya mkataba wake na FC Lupopo.
Ameitaka Yanga kuilipa FC Lupopo pesa zao za mkataba wa mwaka mmoja wa mkopo mwingine ili kuachana na malumbano baina yao huku wakiwa tayari wamejipanga kuelekea mbali zaidi kunako shirikisho la soka dunia fifa na lile la Afrika caf endapo hilo litashindikana.
BOFYA CHINI KUMSIKILIZA KATIBU WA LUPOPO CONSTANTINE KABIKA